1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUfaransa

Baadhi ya shule zafungwa Ufaransa kutokana na kunguni

7 Oktoba 2023

Waziri wa Elimu wa Ufaransa Gabriel Attal ametangaza jana kuwa nchi hiyo imelazimika kufunga shule saba zinazowapokea wanafunzi wapatao 1,500 baada ya kuvamiwa na kunguni.

https://p.dw.com/p/4XETH
Gemeine Bettwanze, Bettwanze, Bett-Wanze, Hauswanze, Haus-Wanze (Cimex lectularius), mit stechend-saugenden Mundwerkzeug
Picha: F. Fox/blickwinkel/imago images

Mapema wiki hii, mamlaka ya Paris ilitangaza kufungwa kwa shule mbili kwa sababu ya kunguni, moja huko Marseille na nyingine Villefranche-sur-Saone nje kidogo ya mji wa kusini mashariki wa Lyon.

Soma zaidiShule zafungwa Ufaransa kutokana na kunguni

Serikali ya Ufaransa imefanya msururu wa mikutano wiki hii kuchunguza idadi inayoongezeka ya visa vya kunguni, wakati nchi hiyo ikiandaa Kombe la Dunia la Rugby na ambayo itakuwa mwenyeji ya Michezo ya Olimpiki hapo mwakani.