Azam yathibitisha kujiengua kwa Kagame Cup
24 Juni 2024Ugumu wa ratiba kwa ajili ya msimu mpya wa ligi na mashindano ya kimataifa ni sababu mojawapo inayotajwa na timu hizo kuomba kujiondoa.
"Kwanini kagame walileta michuano hii Tanzania ni kwa sababu ya mvuto wa timu hizi kubwa ukiangalia viwango vya Simba na Yanga Kimataifa kwa kiasi kikubwa kwa upande mkubwa wanafanya vizuri katika ukanda wa Africa mashariki na kati kujitoa kwao kuna athari ya moja kwa michuano kukosa mvuto na ushindani " Alisema Mchambuzi wa Soka Seleman Kodima.
Soam pia: Kenya bingwa CECAFA, Zanzibar mashujaa
Katika mahojiano na Afisa Habari wa Simba Ahmed Ally amesema "siwezi kuthibitisha moja kwa moja sababu sijajua kitu gani kimeadaliwa sisi Timu inaondoka mwezi wa 7 kwenda Misri sasa kuhusiana na michuano ya CECAFA sijapewa maamuzi ya mwisho ya Klabu tunafanya nini kuhusiana na CECAFA"
Mabingwa wa kagame Cup mwaka 2015 na 2018 Azam FC afisa wa habari Zakaria Thabit amesema "Kambi yetu ya maandalizi ya Msimu mpya inaanza Tarehe 4 kiufundi hauwezi kucheza mechi tarehe 6 hivyo hatutaweza kushiriki katika tarehe hizo tunaheshimu sana haya mashindano ni makubwa sana."
Hata hivyo, Yanga hawajatoa majibu ya moja kwa moja kama hawataashiriki au watashiriki mashindano hayo ambayo wanarekodi ya kutwaa mara tano.
Meneja habari na mawasiliano wa Yanga Ally Kamwe amesema "Kwa sasa bado ofisi ya Mtendaji Mkuu haijakuwa na jibu hilo kwa hiyo wiki hii tutawapa taarifa na kujulisha umma iwapo tutashiriki au hatutashiriki ."
Maandalizi yanaendelea
Mara ya mwisho michuano hii kufanyika ilikuwa mwaka 2021 na ilifanyika Tanzania. Je, maandalizi yamefikia hatua gani afisa habari wa Shirikisho la Mpira wa miguu nchini Tanzania (TFF) Cliford Ndimbo amesema "sisi ni wenyeji kuna vitu vingi haviko tayari tusubiri kwanza CECAFA kwa sababu kuna vitu wanafanya mabadiliko"
Ndimbo amedokeza wanatarajia kujua ni timu gani zimejitoa na timu zipi zimejumuishwa na kwamba mambo mengine yako tayari.
Michuano hii ambayo husirikisha mabingwa wa nchi kutoka ukanda wa CECAFA imerejea mwaka huu 2024 na Timu shiriki zilitangazwa kuwa 16 huku tatu zikiwa ni mwalikwa na 13 zinatokea Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na itaanza kutifua Vumbi kuanzia Julai 6-22.
//Mhindi Joseph