Austria kupata serikali ya kwanza ya mrengo mkali ya kulia?
7 Januari 2025Matangazo
Juhudi za kuunda serikali mpya nchini humo bila ya chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha Freedom Party zilishindikana katika siku za hivi karibuni, zaidi ya miezi mitatu baada ya chama hicho kushinda uchaguzi wa bunge.
Soma pia: Chama cha mrengo wa kulia chashinda Austria
Rais Alexander Van der Bellen jana alimpa jukumu kiongozi wa chama cha Freedom Herbert Kickl kuunda serikali ya mseto katika kipindi cha wiki au miezi kadhaa ijayo.
Chama hicho kiliundwa mnamo mwaka 1956 na wafuasi wa zamani wa utawala wa Manazi na katika kipindi cha miongo kadhaa kimekuwa nguvu kubwa ya kisiasa nchini Austria.