Austin amrai Trump kutoacha kuisaidia Ukraine dhidi ya Urusi
10 Januari 2025Akizungumza katika mkutano wa kundi la mataifa linaloiunga mkono Ukraine, katika kambi ya jeshi la Marekani nchini Ujerumani, Lloyd ameonya kuwa kusitisha msaada wa kijeshi sasa, kutasababisha uchokozi zaidi, machafuko na vita.
''Ni juu ya utawala ujao kufanya maamuzi yao yenyewe. Tunataka kuhakikishiwa kuwa tumefanya kila tuwezalo kuhakikisha tunaendelea kutoa msaada, na wanaweza kuchagua upande wowote wanaotaka kuufata,'' alisema Waziri Austin.
Soma pia: Zelensky: Kurejea kwa Trump ni ukurasa mpya kwa dunia
Wakati huo huo, Trump amesema maandalizi ya kukutana na Rais wa Urusi, Vladimir Putin yanaendelea.
Trump amesema katika mkutano wao watavizungumzia vita vya Ukraine, ingawa taarifa zaidi kuhusu mazungumzo hayo ya ngazi ya juu bado hajizaamuliwa.
Ukraine ina wasiwasi kwamba Trump atakapoingia rasmi madarakani, misaada ya Marekani itapunguzwa sana.