AU yairai Mali kuweka wazi mpango kuelekea demokrasia
13 Aprili 2024Mapema wiki hii utawala wa kijeshi wa Mali uliamuru kusitishwa kwa shughuli zote za kisiasa uamuzi ambao Umoja wa Afrika umesema "unaleta mashaka" na unaweza kuwa kihunzi cha mchakato wa kuirejesha nchi kwenye utawala wa kiaria.
Waziri Mkuu wa Mali, Choguel Kokalla Maiga aliyechaguliwa na majenerali waliompindua Rais Ibrahim Boubacar Keita mwezi Agosti 2020, alisema siku ya Alhamisi kuwa uchaguzi utaandaliwa tu pale taifa hilo litakaporejesha utulivu.
Kwa sasa Mali inaandamwa na ukosefu mkubwa wa usalama unaotokana na hujuma za makundi ya itikadi kali.
Hata hivyo Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat, ameukosoea mwelekeo uliochukuliwa na mamlaka za nchi hiyo na kuzirai ziweke wazi mpango wa kukamilisha kipindi cha mpito.