Wakati mataifa yote ulimwenguni yakitatizika kuzuia ongozeko la joto duniani, madhara ya mabadiliko ya tabianchi tayari yanadhihirika wazi. Ukame, mafuriko, vimbunga, mioto ya misitu vimeharibu maisha ya mamilioni ya watu na kuwaweka katika hatari zaidi ya kukabiliwa na njaa na hata matatizo ya kemkem ya kiafya. Sikiliza makala ya Mtu na Mazingira iliyoandaliwa na Bakari Ubena.