1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Asasi za kiraia Tanzania zapinga kauli kutumiwa na wadhamini

Deo Kaji Makomba25 Oktoba 2021

Asasi za kiraia Tanzania zinazofanya kazi katika sekta mbalimbali nchini humo, ikiwemo elimu, afya mazingira na nyingenezo zimepinga vikali madai kwamba zimekuwa zikitumiwa na mabeberu kwa ajili ya masilahi yao binafsi. 

https://p.dw.com/p/42A6j
Berlin Stolpersteine
Picha: Harrison Mwilima/DW

Kauli hiyo imeibuka katika Kongamano la wiki ya Azaki mwaka 2021 linalofanyika Jijini Dodoma na kuishirikisha Mikoa ya Tanzania Bara  na Zanzibar, likiwa na kauli mbiu isemayo mchango wa Azaki zisizokuwa za kiserikali katika maendeleo ya taifa.

Katika Kongamano hilo lililokuwa likiendeshwa na njia ya majadiliano mada kuu iliyotawala ilikuwa ni kuhusu kauli ambazo zimekuwa zikitolewa kuwa asasi za kiraia zimekuwa zikitumiwa na mataifa ya kigeni, huku baadhi ya asasi hizo zikielezwa kutokuwajibika katika shughuli zao. 

Mkurugenzi wa Azaki ya CSO Francis Kiwanga, katika Kongamano hilo amesema kuwa licha ya kuelezwa kuwepo na changamoto za uwajibikaji katika asasi za kiraia nchini Tanzania, hiyo haina maana kuwa Azaki zote ziko vile.

Wakichangia katika Kongamano hilo wawakilishi wa Azaki kutoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Zanzibar, wamesema kuwa umefika wakati wa kuwa na tafiti maalumu zinazoonyesha umuhimu wa Azaki katika mchango wa maendeleo ya taifa. 

Kongamano hilo lilianza tangu Ijumaa iliyopita huku likiwa na kauli mbiu ya Azaki kwa maendeleo ya taifa.