ARUSHA: Watuhumiwa wa kesi ya vyombo vya habari vya chuki katika mauwaji ya Rwanda ya 1994 kuhukumiwa disemba tatu, na mahakama ya kimataifa-
21 Novemba 2003Matangazo
Hukumu ya watuhumiwa watatu wa mauwaji ya Rwanda ya mwaka 1994, katika kesi inayojulikana kama ya Vyombo vya habari vya chuki, katika mahakama ya kimataifa kuhusu Rwanda yenye makao yake mjini Arusha-Rwanda, itatolewa tarehe tatu mwezi disemba ujao. Watuhumiwa hao ni Bwana Ferdinand Nahimana, aliewahi kuwa Mkurugenzi wa taasisi ya Rwanda ya utangazaji Orinfor, na Jean-Bosco Barayagwiza, aliekua mkurugenzi katika wizara ya mambo ya kigeni, wanatuhumiwa kua miongoni mwa waanzilishi wa Redio RTLM, iliyokua ikichochea mauwaji dhidi ya watutsi. Mtuhumiwa mwingine, Ngeze Hassan, alimiliki gazeti, lililochochea pia chuki za kikabila na mauwaji.