MigogoroAzerbaijan
Armenia yataka kuwepo ujumbe wa UN huko Nagorno Karabakh
24 Septemba 2023Matangazo
Akizungumza kwenye Mjadala Mkuu wa Umoja wa Mataifa mjini New York jana Jumamosi, Mirzoyan amesema jumuiya ya kimataifa na Umoja wa Mataifa zimeshindwa kuwaokoa watu.
Waziri huyo ametoa wito wa kuwepo kwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa utakaofuatilia hali jumla ya haki za binadamu pamoja na usalama katika eneo hilo.
Nagorno-Karabakh ni sehemu ya Azerbaijan lakini sehemu kubwa ya wakaazi wake ni jamii ya Waarmenia. Kwa muda mrefu udhibiti wa eneo hilo umekuwa chanzo cha mzozo kati ya mataifa hayo mawili yaliyokuwa hapo zamani katika Muungano wa Kisovieti.