1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Armenia yalitambua taifa huru la Palestina

21 Juni 2024

Wizara ya Mambo ya Nje ya Armenia imetangaza hii leo kulitambua rasmi taifa huru la Palestina, na hivyo kukaidi matakwa ya Israel ambayo inapingana na hatua kama hizo.

https://p.dw.com/p/4hLw1
Waziri Mkuu wa Armenia, Nikon Pashinyan.
Waziri Mkuu wa Armenia, Nikon Pashinyan.Picha: Alexander Patrin/ITAR-TASS/IMAGO Images

Armenia imesisitiza kuwa inaunga mkono azimio la Umoja wa Mataifa la kusitisha mara moja mapigano katika Ukanda wa Gaza, pamoja na suluhisho la mataifa mawili katika mzozo wa Palestina na Israel.

Soma zaidi: Israel yashambulia katikati ya Gaza, yaingia ndani Rafah

Hayo yanajiri wakati mapigano yakiendelea kuripotiwa huko Gaza ambapo vikosi vya Israel vimeushambulia mji wa Rafah na maeneo mengine katika ukanda huo, vikidai ni katika kuendeleza azma yao ya kutaka kulitokomeza kabisa kundi la Hamas.