1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Annalena Baerbock afanya ziara Mashariki ya Kati

5 Septemba 2024

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock yupo nchini Saudi Arabia ambapo atarajiwa kufanya mazungumzo kadhaa juu ya hali ya Mashariki ya Kati.

https://p.dw.com/p/4kIiO
Saudi-Arabia | Annalena Baerbock ziarani mjini Riadh
Baerbock anatarajiwa kuweka uzito zaidi katika kuendelezwa kwa mazungumzo juu ya kusimamishwa mapiganoPicha: Thomas Koehler/AA/photothek.de/picture alliance

Waziri Baerbock pia atakwenda Jordan, Israel na Ukingo wa Magharibi unaokaliwa na Israel.

Waziri huyo wa Ujerumani anatarajiwa kuweka uzito zaidi katika kuendelezwa kwa mazungumzo juu ya kusimamishwa mapigano na kuachiwa kwa mateka wa Israel waliobakia.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani ameeleza kuwa waziri Baerbock na mwenyeji wake wa Saudi Arabia Faisal bin Farhan Al-Saud, watazungumza juu ya hali tete katika Mashariki ya Kati.   

Wakati huo huo Israel imefanya mashambulio kwenye Ukingo wa Magharibi.

Kwa mujibu wa taarifa ya shirika la habari la Palestina WAFA, watu watano wameuawa katokana na shambulio la droni kwenye mji wa Tubas.