1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANKARA : Uturuki yatakiwa kuboresha haki za binaadamu

6 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CEUW

Mkuu wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia masuala ya kutanuka kwa umoja huo Olli Rehn amekutana na waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Abdulla Gul leo hii na kusisitiza kwamba Uturuki lazima iendelee kuboresha haki za binaadamu na kuimarisha utawala wa sheria wakati ikisonga mbele na mazungumzo ya kuwa mwanachama wa umoja huo.

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamesisitiza kwamba kuingia kwa Uturuki kwenye Umoja wa Ulaya sio jambo la uhakika licha ya kuanza hapo Jumatatu kwa mazungumzo ya nchi hiyo kujiunga na umoja huo.Mazungumzo ya nchi hiyo kuwa mwanchama wa umoja huo yanaweza kuchukuwa miaka 10 hadi 15.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Ankara Rehn amesema Uturuki itakuwa chini ya uchunguzi mkali na ili ikamilishe mazungumzo hayo na kuwa mwanachama itabidi ikidhi kikamilifu sifa za kisiasa za umoja huo.