Angola yaituhumu M23 kwa kukiuka usitishaji mapigano Kongo
23 Oktoba 2024Matangazo
Taarifa iliyochapishwa wiki hii na serikali ya Angola imesema udhibiti wa mji wa Kalembe Jumapili iliyopita na vikosi vya M23 ni ukiukaji wa wazi wa mpango wa usitishaji mapigano. Taarifa hiyo iliongeza kuwa serikali ya Angola inapinga na inalaani vikali kitendo hicho cha uhasama, ambacho kinakiuka juhudi zinazoendelea za kutafuta suluhisho la kudumu kwa mzozo huo. Makubaliano ya kuweka chini silaha kati ya Kongo na waasi wa M23yamekuwepo tangu mapema Agosti kufuatia mchakato wa upatanishi uliosimamiwa na Angola. Lakini makabialiano Jumapili kati ya M23 na wapinagaji wanaoiunga mkono serikali wakijiita Wazalendo katika mji wa Kalembe wa mkoa wa Kivu Kaskazini yalivunja mpango huo.