Angola yahitaji sare leo na Tunisia.
31 Januari 2008DEUTSCHE WELLE 31-01-08
Autor:Ramadhan Ali
Title: Sports-Africa Cup
Journal II.
Mod.
Duru ya kwanza ya Kombe la Afrika la Mataifa nchini Ghana inakamilika leo kwa mapambano 2: Bafana Bafana Afrika kusini ina miadi na simba wa terange-Senegal mjini Kumasi wakati Tunisia inaonana na Angola mjini Tamale.
Angola leo inahitaji suluhu na pointi 1 kuingia kwa mara ya kwanza robo-finali ya kombe la Afrika la mataifa wakati maadui zao Tunisia-mabingwa 2004,pia watatosheka na sare kusonga mbele wakati simba wa Terange-senegal wanategemea ukarimu ama wa Angola au wa tunisia kuibuka na ushindi na kuwafungulia wao mlango wa duru ijayo.
Senegal wako nafasi ya 3 katika kundi lao wakiwa na pointi 1 ,lakini wakiitimua leo Afrika kusini mjini Kumasi watasonga mbele mradi tu mapambano hayo mengine hayamailiziki sare.
Senegal itaongozwa leo na kocha mpya-nae ni Lamine N’Diaye-hii ni kwa kuwa kocha wao mpoland Henri Kasperzack alijiuzulu majuzi baada ya Senegal kukandikwa mabao 3-1 na Paa wa Angola.
Mabingwa watetezi-Misri walikata jana tiketi yao ya robo-finali licha ya kutoka sare bao 1:1 na Chipolopolo-Zambia.Amr Zaki alilifumania lango la Zambia tayari mnamo dakika ya 16 ya mchezo,lakini christopher Katongo,alisawazisha dakika 2 kabla ya firimbi ya mwisho kulia.
Simba wa nyika-Kameroun wanaifuata kwahivyo,Misri duru ijayo baada ya samuel Eto’o –simba wao dume kulifumania jana mara mbili lango la Sudan na kutia bao lake la 15 na 16 katika historia ya Africa Cup.Kwa mabao hayo 2, Samuel Eto’o jana aliifuta kabisa kitabuni rekodi ya Muivory Coast Laurent Pokou ya mabao 14 na sasa ni yeye alienyakua rekodi ya mtiaji magoli mengi kabisa katika historia ya kombe la Afrika.