Angola kujiondoka katika mataifa ya OPEC
22 Desemba 2023Matangazo
Waziri wa mafuta wa taifa hilo la Kiafrika Diamantino de Azevedo, amesema Angola haifaidiki na chochote kwa kubaki katika shirika hilo. Nchi hiyo ilijiunga na OPEC katika mwaka wa 2007. Angola inasema sera za OPEC hazitumiki tena kwa maslahi yake ya kuepuka kushuka kwa uzalishaji na kuheshimu kandarasi. Angola na Nigeria, nchi mbili zinazozalisha mafuta kwa wingi katika eneo la kusini mwa jangwa la Sahara, zilipinga uamuzi huo wa OPEC. Nchi hizo zinataka kuendeleza uzalishaji kama chombo cha kupata fedha za kigeni. OPEC, kundi lenye wanachama 13 lililoanzishwa mwaka wa 1960, liliongeza wanachama wapya 10 katika mwaka wa 2016 chini ya jina la OPEC+, katika juhudi ya kutaka nguvu zaidi.