1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Angola katika Kombe la Afrika huko Ghana

14 Januari 2008

Angola inajiwinda kuwasangaza mahasimu wao Tunisia,Afrika Kusini na Senegal.

https://p.dw.com/p/CpXb
Mshambiliaji maarufu DroghaPicha: pa / dpa

Ghana –wenyeji wanafungua dimba la kombe la 26 la Afrika la mataifa jumapili hii ijayo wakicheza na jirani zao Guinea,mjini Accra.

Angola ndio wenyeji wa kombe lijalo la Afrika baada ya Ghana,miaka 2 kutoka sasa 2010-mwaka pia wa Kombe la kwanza barani Afrika nchini Afrika Kusini.

Mashabiki wa afrika nao wameshaanza kutakasa masikio na kutega macho yao mjini Accra wakijuliza timu kama Angola,Zambia,Sudan au Mali zaweza kuzitia munda timu kubwa kama Ghana,Nigeria,kameroun,Senegal au mabingwa Misri ?

Angola ,ambayo haikuaibisha Afrika hapa Ujerumani katika kombe la dunia na ilitoa changamoto kali mjini Cologne ilipokumbana na Ureno,mkoloni wake wa zamani, ina azma ya kupiga hatua moja zaidi katika kombe hili la Afrika kabla kuandaa binafsi hilo lijalo nyumbani 2010.

„PAA WEUSI“ –Black Antelopes hawa wamepkua wakipiga hatua kwa hatua wakisonga mbele kila waliposhiriki katika kombe hili mara 3 zilizopita.

1966,Angola, iliondoka na pointi moja tu,miaka 2 baadae ikarudi nyumbani na pointi 2 na mwaka 2006-mwaka ilipokuja katika kombe la dunia hapa Ujerumani,ilizidisha pointi hizo zikawa 4.

Angola inatoa maanani nafasi zao za kuwika katika kombe hili alao hadharani,kindani ndani lakini paa wamepania kweli kuwasangaza tai wa Carthage-Tunisia,halafu senegal-simba wa tarange kabla hwajachuana na majirani zao Bafana bafana katika zahama za kundi hili ambalo kila timu ina nafasi ya kuiangusha nyengine.

Angola itapata taabau mbele ya tunesia,kwani ni timu yenyer maarifa na uzoefu mkubwa katika kombe hili na kombe la dunia.

IOna mastadi wengi zaidi kuliko Angola wanaocheza katika Ligi ya Ulaya.Kwahivyo itakua shabaha ya angola huko ghana kuinyima ama Senegal au Afrika kusini nafasi ya pili kutoka kundi lao ili kukata tiketi ya duru ya pili ya kombe hili.

Angola ina mastadi wa kujivunia na wanaoinukia:washambulizi wake Flavio Amado na Manucho Concalves watakaojiunga na Manchester United baada ya kombe hili la afrika nchini Ghana endapo wakijipatia ruhusa za kazi, ndio ufunguo wa Angola kuvunja tumbuu za milango ya Bfana Bafana,tai wa Carthage na ya pori la simba wa tarange-Senegal wiki ijayo.

Angola itategemea zaidi mastadi wake wengi walioteremka hapa Ujerumani kwa kombe la dunias 2006 na wengi wao bado imara:Angola itawakosa tu akina Joao Ricardo-kipa wao alietamba katika kombe la dunia na mshambulizi wao Fabrice „Akwa“ Maieco aliestaafu katika timu ya taifa.

Homa kwahivyo, imewaingia mashabiki wa Angola kama ilivyowaingia mashabiki wa nchi jirani kuanzia kusini mwa Afrika ambako mbali na Angola, zashiriki ,Zambia ,Namibia na Afrika Kusini lakini hata Afrika mashariki na kati.