Angela Merkel: Miaka 16 kama Kansela wa Ujerumani
Angela Merkel amekuwa Kansela wa Ujerumani tangu mwaka 2005. Haya ni baadhi ya matukio muhimu katika uongozi wake wa muda mrefu ulioiongoza kufanya mabadiliko makubwa.
Mwanasiasa Hodari
Kansela wa zamani Helmut Kohl na viongozi wengine wa kisiasa walimfahamu Merkel kama Mwanasiasa hodari. Mwaka 2001 alikiongoza chama cha Christian Democrats akiwa upande wa upinzani. Lakini mambo yakabadilika mwaka 2005.
Ushindi Mwembamba
Katika uchauzi wa mwaka 2005 CDU pamoja na chama ndugu cha Bavaria CSU vilishinda na kukiacha nyuma chama cha siasa za wastani za mrengo wa kushoto SPD kilichoongozwa na Kansela Gerhard Schröder.
Kansela mpya
Vyama vya CDU na SPD viliunda serikali ya muungano, na Merkel akawa mwanamke wa kwanza, mtu wa kwanza anayetokea mashariki mwa Ujerumani na mwanasayansi wa kwanza kuwa Kansela na mtu aliye na umri mdogo kushikilia nafasi hiyo.
Mwenyeji wa wengi
Merkel mara moja akaonyesha kuwa mchapa kazi. Katika mkutano wa G8 mwaka 2007 akawakaribisha mjini Heiligendamm, iliyoko katika bahari ya Baltic, viongozi wa mataifa 8 yenye nguvu zaidi kiuchumi duniani. Alitaniana na Rais wa Marekani George W. Bush (kushoto) na rais wa Urusi Vladimir Putin (kulia).
Wanaume kama wanaume
Katika jukwaa la kisiasa barani ulaya, Mwaka 2008 Merkel alikutana na viongozi wa kiume walio na kiburi, rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy (mbele) na Waziri Mkuu wa Italia Silvio Berlusconi. Ukuaji wa mgogoro wa kifedha ukawa jambo linaloupa wasiwasi Umoja wa Ulaya.
Saidia au zuwiya?
Madeni yaliyoyakabili baadhi ya mataifa ya Umoja wa Ulaya yakaongezeka na kutishia kupotea kwa sarafu ya euro. Merkel akaamua kusaidia kwa kuja na mpango wa kubana matumizi. Hilo halikupokewa vizuri hasa nchini Ugiriki, ambako magazeti yalikuwa na picha zinazofananisha hali iliyokuwepo na uongozi wa kinazi katika vita vya pili vya dunia.
Kampeni iliyosita
Merkel sio mzungumzaji mzuri, Hotuba zake sio ndefu na hakugusii sana kwa kina masuala ya sera. lakini ukimya wake, utulivu na unyenyekevu umemfikisha mbali na kumfanya kupendwa na wengi, hatua iliyomuwezesha kuongoza serikali nne.
Mama
Wakati mmoja katika uongozi wake wa muda mrefu, Merkel akavikwa kofia mbili. Kansela wa nchi na mama wa taifa. Wafuasi wake na wapinzani wake walimuita Mama. Neno hili linaweza kuchukuliwa kidogo kidhihaka lakini pia ni la upendo zaidi.
'Tunaweza'
Taarifa zake chache zimekuwa na neno hili "tunaweza" alipongezwa sana mwaka 2015 kwa kushikilia dhamira yake ya sera ya Umoja wa Ulaya ya kuyaweka mipaka wazi, na kuruhusu zaidi ya wakimbizi na wahamiaji milioni moja, wengi wakitoroka vita Syria kuingia Ujerumani na maeneo mengine ya Umoja huo. Watu wachache walimpiga Merkel kwa hatua aliyoichukua.
Time's 'Mtu wa mwaka'
Gazeti la Times, lilimtaja Merkel kama mtu muhimu wa mwaka 2015 na hata kansela wa dunia iliyo huru. Alionyesha ujasiri katikati ya migogoro tofauti, kifedha kijamii na kisiasa.
Mfano wa Busara
Merkel ni msiri. Ni mkimya katika fikra zake binafsi na viongozi asiyowakubali. Lakini anafanya nao kazi kwa masilahi ya taifa.
Asiyependa Makuu
Merkel anajua bei ya vitu madukani. Miaka mingi ya kuiongoza nchi haijaonekana kumpanda kichwani na kumfanya mtu aliye na kiburi au majivuno. Hapa mwaka 2014 alitembelea duka moja mjini Berlin akiwa na Waziri Mkuu wa China Li Keqiang. Sio kawaida kukutana na kansela akinunua vitu madukani mjini Berlin.
Almasi ya uaminifu
Merkel anajulikana sana kwa kukunja mikono yake kuifanya kama shepu hii ya almasi. Alisema inamsaidia kusimama wima. Chama cha CDU kilitumia ishara hiyo katika makaratasi ya kampeni zake katika uchaguzi wa mwaka 2013. Kikajulikana kwa uaminifu na utulivu
Maisha yake binafsi
Merkel ni mtu binafsi sana. Dunia haijui mengi kumuhusu isipokuwa kwamba mume wake, Joachim Sauer, pia ni mwanasayansi. Wawili hao wanapenda kusherehekea siku kuu ya pasaka katika kisiwa cha Ischia, Italia.
Janga la COVID 19
Janga la corona limebadilisha mambo mengi nchini Ujerumani. Ujerumani na mataifa mengine yakamuomba ushauri Merkel juu ya janga hilo. Mtindo wake wa kuongoza kwa umakini na uwazi ulimmpa umaarufu.
Kwaheri Bibi Merkel
Miaka miwili iliyopita, Merkel aliweka wazi kwamba hatogombea tena ukansela mwaka 2021. Merkel ameitumikia Ujerumani kwa miaka 16. Rekodi hii inalingana na mshauri wake Helmut Kohl, Kansela aliyeongoza kwa muda mrefu.