Andrich asaini mkataba mpya wa kusalia Leverkusen hadi 2028
16 Agosti 2024Kiungo wa kati wa Ujerumani Andrich ameongeza mkataba wa kuitumikia Leverkusen hadi 2028.
Kiungo huyo ameichezea timu ya taifa ya Ujerumani kwa mara ya kwanza mwezi Novemba mwaka jana na tangu wakati huo ameichezea timu ya taifa michezo 10, na kujumuishwa kwenye kila mechi ya timu hiyo katika michuano ya Euro 2024.
Msimu uliopita, Leverkusen ilikuwa timu ya kwanza katika historia ya Bundesliga kucheza mechi zote za msimu bila kushindwa, na kushinda taji lao la kwanza la ligi ya Bundesliga.
Soma zaidi. Bayer Leverkusen kukipoiga na Stuttgart DFL-SUPER CUP
Katika taarifa, Andrich alisema Leverkusen ilikuwa ni "anwani sahihi kabisa.
"Ninapitia kipindi cha mafanikio zaidi cha maisha yangu na ninahisi njaa ya timu bado ni kubwa hata baada ya msimu huu maalum."
Mkurugenzi wa michezo wa Leverkusen Simon Rolfes alimwita Andrich "nguzo kuu" ya klabu huku akisifia "uchezaji wake bora kwenye jukwaa la kimataifa".
Leverkusen watafungua msimu wao katika Kombe la Super Cup la Ujerumani Jumamosi hii, wakiwakaribisha Stuttgart.