ANC yazidi kupoteza uungaji mkono - Utafiti
24 Mei 2024Kulingana na uchunguzi wa maoni uliofanywa na shirika la Social Research Foundation (SRF), chama cha ANC kimeshuka kutoka asilimia 45.9 hadi 40.9 ndani ya wiki moja tu, kufuatia maoni ya asilimia 60 ya wapiga kura.
Soma zaidi: Afrika Kusini yaadhimisha miaka 30 ya demokrasia
Hata hivyo, bado chama hicho, ambacho kimekuwa madarakani kwa miongo mitatu, kinapigiwa upatu kuibuka kuwa chama kikubwa katika uchaguzi huo wa Mei 29, lakini kwa mara ya kwanza, kinaweza kupoteza viti vingi bungeni.
Soma zaidi: Ramaphosa atafuta kura kwa Waafrika Kusini baada ya miaka 30 ya utawala wa ANC
Wiki iliyopita, Rais Cyril Ramaphosa alisaini sheria mpya inayolenga kutoa huduma ya afya kwa umma, licha ya pingamizi kutoka vyama vya upinzani na makundi ya wafanyabiashara.
Baadhi ya wachambuzi wanaamini hatua hiyo imechangia kuporomoka kwa uungwaji mkono wa chama.