1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Amnesty yatoa wito kuachiwa wanaharakati wawili Afghanisatn

4 Februari 2024

Shirika la utetezi wa haki za binaadamu la Amnesty International limetoa wito wa kuachiwa bila ya masharti wanaharakati wawili wa elimu wa Afghanistan ambao walikamatwa na vikosi vya usalama vya Taliban mjini Kabul.

https://p.dw.com/p/4c1cQ
Haki za Binadadu | Agnes Callamard  Katibu Mkuu wa Amnesty International
Agnes Callamard, Katibu Mkuu wa Amnesty International.Picha: Carlos Garcia Granthon/ZUMA Press/picture alliance

Katika taarifa yake iliyotolewa Ijumaa jioni, Amnesty International imedai, Ahmad Fahim Azimi na Seddiqullah Afghan, wanaharakati wanaofanya kazi na shirika la elimu Fekre Behtar, wamekamatwa kiholela.

Tangu kurejea madarakani, serikali ya Taliban inatajwa kubinya haki za watu nchini humo. Shirika, Amnesty liliongeza kwa kusema kukamatwa kwa watu hao ni kinyume na sheria ya kimataifa ya haki za binadamu. 

Soma pia:Amnesty yataka Afghanistan kuwaachia wanaharakati 2

Nchini Afghanistan wasichana na wanawake hawaruhusiwi kusoma zaidi ya shule ya msingi na vikosi vya Taliban vinalaumiwa kwa ukandamizaji dhidi ya wapinzani.