Amnesty: Sheria ya usalama imeangamiza uhuru Hong Kong
30 Juni 2021Haya yanakuja mwaka mmoja baada ya China kutangaza sheria hiyo mjini humo. Sheria hiyo kali ya usalama wa kitaifa -- ambayo inafanya kuwa uhalifu kitu chochote ambacho mamlaka zitakiona kuwa cha kuhujumu serikali, kutaka kujitenga, kula njama na mataifa ya kigeni na ugaidi ikiwa na adhabu ya kifungo cha maisha ya jela -- imebadilisha pakubwa mazingira ya kisiasa na kisheria ya Hong Kong.
Mkurugenzi Mkuu wa Amnesty International kanda ya AsiaPasifiki Yamini Mishra amesema sheria hiyo imeiweka Hong Kong kwenye mkondo wa kuwa dola la kipolisi. Beijing ilisisitiza kuwa sheria hiyo ilihitajika kurejesha utulivu baada ya maandamano makubwa na wakati mwingine yenye vurugu ya kudai demokrasia mwaka wa 2019 lakini ikaahidi kuwa itawalenga tu wenye itikadi kali.