Amnesty International yaishtumu Israel kwa mauaji ya halaiki
5 Desemba 2024Shirika hilo limesema Israel imefanya hivyo kuwa kutaka kuwaangamiza kwa makusudi Wapalestina kwa kufanya mashambulizi makali, kubomoa miundombinu muhimu na kuzuia kupelekwa kwa chakula, dawa na misaada mingine katika Ukanda wa Gaza.
Amnesty International leo limetoa ripoti katika Mashariki ya Kati ambayo inasema hatua kama hizo haziwezi kuhalalishwa na shambulio la Hamas la Oktoba 7, 2023 dhidi ya Israeli, ambalo lilichochea kuzuka kwa vita hivyo, ama pia uwepo wa wanajeshi katika maeneo ya raia.
Soma pia:UN: Hali ya Gaza ni ya kutisha na ni janga kubwa
Mkuu wa shirika hilo Agnès Callamard amesema, ''Taifa la Israel limefanya na linaendelea kufanya mauaji ya halaiki dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza tangu tarehe 7 Oktoba 2023 siku ambayo Hamas ilifanya uhalifu wa kutisha dhidi ya raia wa Israel na watu wengine. Hiyo ni zaidi ya mwaka mmoja uliopita. Wapalestina wa Gaza wamekuwa wakiishi na hofu siku baada ya siku, mauaji makubwa yametokea mbele yao na ulimwengu, na hakuna dalili ya kumalizika.''
Kulingana na shirika hilo, Marekani na washirika wengine wa Israel wanaweza kuhusishwa na mauaji ya halaiki, na kuwataka kukoma kuipa silaha Israel.