1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa zamani wa Kenya ashtakiwa kwa ubadhirifu wa fedha

23 Desemba 2023

Tume ya kupambana na ufisadi nchini Kenya, imemfungulia mashtaka waziri wa zamani wa utalii Najib Balala pamoja na watu wengine wawili kwa mashtaka ya wizi wa mamilioni ya dola ya ujenzi wa chuo cha utalii

https://p.dw.com/p/4aWRy
Mahakama ya juu ya Kenya
Mahakama ya juu ya KenyaPicha: Yasuyoshi Chiba/AFP

Balala, katibu mkuu wa zamani Leah Addah Gwiyo, na msimamizi mshirika wa kampuni ya West Consults, John Odero, walifikishwa mbele ya hakimu mkuu James Mwaniki hapo jana mjini Malindi, ambapo walikanusha mashtaka hayo.

Balala ni waziri wa kwanza wa zamani kufunguliwa mashtaka chini ya serikali ya Ruto

Balala ni mtu wa kwanza maarufu aliyekuwa akishikilia wadhifa mkubwa serikalini kushtakiwa kwa ufisadi chini ya utawala wa Rais William Ruto. Watatu hao waliachiliwa kwa dhamana.

Washukiwa wengine 13 wanatarajiwa kufunguliwa mashtaka ya ufisadi kwa madai ya ubadhirifu huo uliofanyika miaka 16 iliyopita.

Wakati huo, Balala alikuwa waziri katika serikali ya marehemu Rais Mwai Kibaki.