Aliyekua mpiga picha wa Mandela afariki dunia
2 Januari 2024Chama cha waandishi wa habari wa Afrika Kusini (SACEF) kimeandika, Magubane alifariki dunia huku akiwa amezungukwa na watu wa familia yake.Enzi za uhai wake, Magubane kwa miongo kadhaa alikua akipiga picha zilizoyaanika madhila waliyofanyiwa Waafrika Kusini, ikiwemo ghasia za Soweto za mwaka 1976, ambapo alinasa picha zilizowashangaza wengi kuhusu uasi wanaofanyiwa wanafunzi. Magubane pia aliwahi kufanya kazi na jarida linaloandika utamaduni wa watu weusi la Drum, kabla hajajikita zaidi kwenye masuala ya ubaguzi wa rangi na mapambano dhidi ya usawa. Kazi yake iliyomfanya afungwe zaidi ya mara moja, ambapo mwaka 1969 alikamatwa alipokua akiripoti kuhusu maandamano mbele ya gereza alilokua amefungwa Mandela akahukumiwa kifungo cha siku 586, na mwaka 1971 alishikiliwa tena kwa miezi kadhaa, jambolililomfanya afanye kazi hiyo huku akiwakwepa polisi.Waziri wa Utamaduni wa Afrika Kusini, Zizi Kodwa kupitia mitandao ya kijamii ameandika, taifa lao limempoteza mpigania uhuru wa kweli na msimuliaji hodari wa hadithi alieandika bila woga masuala ya ubaguzi wa rangi.