1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Algeria yataganza serikali mpya

3 Januari 2020

Waziri mkuu wa Algeria Abdelaziz Djerad ameteua baraza jipya la mawaziri siku ya Alhamisi, na kuwabakisha mawaziri kadhaa muhimu katika nyadhifa zao za sasa. Serikali pia imewaachia waandamanaji 76 waliokuwa kizuwizini.

https://p.dw.com/p/3VgwG
Algerien Anti-Regierungsproteste trotz dreitägiger Staatstrauer
Picha: picture-alliance/AP Photo/T. Doudou

Rais Abdelmajid Tebboune alichaguliwa mwezi uliopita na sasa ameanza jukumu la kuwateua viongozi watakaounda serikali ya Algeria.

Tebbune alimemteua Abdelaziz Djerad kama waziri mkuu siku ya Jumamosi, huku nafasi kadhaa za uongozi zikisalia na viongozi walewale kabla ya kuchaguliwa kwake kama rais hatua ambayo inaashiria muendelezo wa sera kuu za serikali ya Algeria.

Abderrahmane Raouia aliteuliwa tena kama waziri wa fedha baada ya kutumikia nyadifa huo tangu mwaka 2017 hadi mwisho wa mwezi  Machi wakati alipobadilishwa.

Tebboune alishinda uchaguzi wa rais kwa asilimia 58 uamuzi ambao waandamanaji waliupinga kwa kuwa idadi ya waliojitokeza kushiriki katika zoezi la upigaji kura ilikuwa asilimia 40 tu.

Aitisha mazungumzo na waandamanaji

Rais huyo ameitisha mazungumzo na waandamanaji hao ambao hawana kiongozi, na wanaendeleza maandamano licha ya kuchaguliwa kwa Tebbounne.

Kipato kikubwa cha Algeria ni mauzo ya nishati na inategemea mafuta na gesi lakini kiwango cha mauzo kimezorota tangu bei zilipoanza kushuka.

Algerien Abdelmadjid Tebboune, neu gewählter Präsident
Rais Abdelmadjid Tebboune.Picha: Reuters/R. Boudina

Serikali ya mpito ilimteua mkuu mpya wa shirika la mafuta la serikali Sonatrach, Kamel Edine Chikhi, pamoja na  gavana mpya wa benki kuu Benabderahmane Ayman, mnamo Novemba.

Waziri wa mambo ya kigeni Sabri Boukadoum, waziri wa nishati Mohammed Akrab na waziri wa ndani Kamel Bedjoud wamesalia katika nyadhfa zao.

Hata hivyo nafasi muhimu katika serikali ya Algeria ya Waziri wa Ulinzi bado ipo wazi baada ya kifo cha Gaed Salah wiki iliyopita.

Bunge pia lilipitisha sheria mpya ya nishati ambayo inalenga kuboresha uwekezaji wa kimataifa katika mafuta na gesi kuwa ya kuvutia wawekezaji zaidi katika ngazi za kimataifa ili kuimarisha soko.

Wakati huo huo serikali imemwachilia Lakhdar Bouregaa, mkongwe wa vita vya miaka ya 1960 vya uhuru ambaye alitiwa kizuizini mnamo Juni na kupelekea kustaafu kwa Hocine Benhadid.

Awali uchaguzi ulikuwa umehairishwa na mkuu wa Jeshi Ahmed Gaed Salah, ambaye alifariki ghafla wiki iliyopita kutokana na mshtuko wa moyo.

Chanzo: rtre,dpa