Algeria yamuapisha rais mpya anayepingwa na waandamanaji
19 Desemba 2019Matangazo
Taifa hilo la Kaskazini mwa Afrika lenye utajiri wa gesi, limemuapisha Tebboune kuwa rais hii leo. Wajumbe wa serikali ya Algeria wanaimani kwamba, Tebboune ataisaidia nchi kurejesha utulivu baada ya miezi 10 ya maandamano ya amani lakini yenye kutishia uhalali wao na kuathiri uchumi.
Tebboune aliye na umri wa miaka 74 na ambaye ana ukaribu na kiongozi wa kijeshi aliye na nguvu nchini Algeria, amewaeleza wana vuguvugu la maandamano la Hirak kuwa katiba inatoa haki ya kuandamana.
Katika hotuba yake ya kwanza kama rais, ameahidi kushughulikia ufisadi ambao unalalamikiwa na waandamanaji na kupunguza mamlaka yake.