JangaTanzania
Ajali 1,735 za barabarani zilitokea Tanzania 2024
3 Januari 2025Matangazo
Kwa mujibu wa jeshi hilo, ajali 1,198 kati ya hizo zilisababisha vifo katika kipindi hicho.
Takwimu za jeshi la polisi zinaonyesha kuwa kwa mwaka 2023, matukio ya ajali za barabarani yalikuwa 1,733 katika kipindi cha Januari hadi Desemba, na kusababisha vifo 1,118.
Soma pia: Watu 22 wapoteza maisha ajali ya basi nchini Brazil
Katika salamu zake za mwaka mpya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Mambo ya Ndani, Innocent Bashungwa, pamoja na Jeshi la Polisi kuongeza mikakati ya kuzuia ajali hizo za barabarani.