1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ai Weiwei aachwa huru

Sekione Kitojo23 Juni 2011

Maafisa wa China wamemuacha huru msanii maarufu na mpinzani nchini humo Ai Wei wei kwa dhamana. Ai ameachwa huru kwasababu za kiafya na kukiri kukwepa kulipa kodi kwa mujibu wa maafisa hao.

https://p.dw.com/p/11hzV
Mwanaharakati msanii Ai Weiwei,kulia, akisalimiana na waandishi habari wa kigeni mara baada ya kuachiliwa.Picha: AP

Maafisa nchini China wamemuacha huru msanii maarufu na mpinzani Ai Weiwei kwa dhamana. Shirika la habari la serikali Xinhua limeripoti kuwa Ai , aliachiliwa huru kwasababu amekiri madai ya kukwepa kulipa kodi pamoja na sababu za kiafya. Serikali za mataifa ya magharibi zimeelezea kuridhishwa kwao na taarifa hizo baada ya kutoa wito wa kuachiwa kwa Ai tangu alipokamatwa Aprili mwaka huu , baada ya hatua kubwa ya serikali ya kamata kamata dhidi ya wapinzani mwaka huu. Mtaalamu wa masuala ya uhusiano wa kimataifa Enerhard Sandschneider amesema kuachiwa kwa Ai kumekuja muda mfupi kabla ya ziara inayopangwa ya waziri mkuu wa China Wen Jiabao katika mataifa ya Ulaya. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema kuwa kuachiwa kwa Ai kunapaswa kuwa hatua ya kwanza tu, na China inapaswa sasa kuielezea dunia kuhusu kukamatwa kwake katika hali ya uwazi.