1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Agathon Rwasa ndiye atakaegombea urais kwa upinzani Burundi

17 Februari 2020

Chama rasmi cha upinzani Burundi kimemchagua kiongozi wa zamani wa waasi na mpinzani wa rais anayeondoka madarakani, Pierre Nkurunziza, Agathon Rwasa, kama mgombea wake katika uchaguzi ujao wa urais.

https://p.dw.com/p/3Xt0I
Agathon Rwasa
Picha: Esdras Ndikumana/AFP/Getty Images

Rwasa sasa atasimama katika uchaguzi huo wa Mei 20 kwa tiketi ya chama hicho cha National Congress for Liberty.

Rwasa alikuwa kiongozi mkuu wa upinzani katika chaguzi mbili zilizopita, ingawa aligomea chaguzi za mwaka 2010 na 2015, akisema wafuasi wake walikuwa wanakandamizwa mno. Chaguzi zote hizo zilishindwa na Nkurunziza.

Uchaguzi wa mwaka 2015 ulisababisha maandamano yaliyopelekea jaribio la mapinduzi liliofanywa na wasioridhishwa na hatua ya Nkurunziza kuongeza muda wake na kutawala kwa muhula wa tatu.

Jeshi la Burundi lilitibua jaribio hilo la mapinduzi na waliohusika wamefungwa au wanakabiliwa na mashtaka.