1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika yataka ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya wageni kuwa makosa ya jinai

Mohamed Dahman27 Agosti 2008

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe kuunda serikali mpya hivi karibuni lakini amesema chama kikuu cha upinzani MDC hakitaki kujiunga na serikali hiyo mpya.

https://p.dw.com/p/F5yh
Ulimwengu unaiangalia tena Afrika safari suala ni ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya raia wa kigeni.

Kauli yake hiyo inakuja wakati ikithibitisha kwamba mazungumzo ya kushirikiana madaraka bado yanaendelea na chama cha MDC kikisema kwamba kimejifunga na mazungumzo hayo ambayo yatakayopelekea kuundwa kwa serikali ya kitaifa.

Gazeti la serikali la The Herald limemkariri Mugabe akiwaambia maafisa wa serikali baada ya kulifunguwa bunge kwamba hivi karibuni wataunda serikali na inaonekana MDC haitaki kuingia kwenye serikali hiyo.

Mugabe ambaye alizomewa wakati akifunguwa bunge na wabunge wa upinzani amesema bado ana matumaini ya kufikiwa kwa makubaliano katika mazungumzo ya kushirikiana madaraka na Morgan Tsvangirai kiongozi wa MDC yenye lengo la kukomesha mzozo wa kisiasa kufuatia uchaguzi tata.

Gazeti la The Herald pia limemkariri Mugabe akilishutumu vikali baraza lake la mawaziri lililopita ambalo amesema ni baya kabisa kuwahi kushuhudiwa katika historia kwamba mawaziri wake wamekuwa wakijali maslahi yao tu na hawaaminiki ingawa sio wote.

Chama cha MDC kimesema kinaendelea kujifunga na mazungumzo hayo lakini kimesisitiza kwamba serikali itakayoundwa iwe ya kitaifa kwa kujumuisha wahusika wote.

Msemaji wa chama cha MDC Nelson Chamisa amesema wana imani na mazungumzo hayo na wamejifunga na mchakato wa mazungumzo hayo ambayo yatatowa matokeo yanayokubalika kwa wahusika wote isipokuwa wanapinga maamuzi ya upande mmoja na kiburi.

Amesema huo ni ushindi kwa ajili ya demekrasia.Ni msimamo wa raia wa Zimbabwe dhidi ya ZANU- PF na hali ilioko na ni ishara kamili kwamba watu wa Zimbabwe wanataka mabadiliko na mafanikio na pia ni tamko linaloashiria kwamba watu wanataka majadiliano hayo yafanikiwe.

Spika wa bunge la Zimbabwe Lovemore Moyo amesema mazungumzo hayo yalioanza mwezi mmoja uliopita bado yamekuwa yakiendelea.

Moyo ambaye ni afisa mwandamizi wa chama cha MDC ameiambia radio moja ya Afrika Kusini kwamba mazungunzo yanaendelea pia amesema kuhanikiza kwa Mugabe ni jambo la kusikitisha pia ameelezea kukatishwa tamaa kwa MDC kutokana na kukwama kwa mzozo huo wa kisiasa nchini humo.

Siphamadia Zondi wa Tasisi ya Global Dialogue anasema nguvu iliomo mikononi mwa MDC wakati wakirudi kwenye mazungumzo kuhusu kushirikiana madaraka makuu ya uongozi ni kwamba watakuwa na kitu fulani cha kutumia katika kujadiliana kwa ajli ya kukabidhiwa kwa madaraka makubwa kwa wadhifa wa waziri mkuu.

Kukwama kwa mazungumzo kati ya Mugabe na Tsvangirai juu ya namna ya kushirikiana madaraka kumedhoofisha matumaini ya kufikiwa kwa makubaliano ambayo huenda yakaiwezesha Zimbabwe kuinuka tena kufuatia kuzorota kwa uchumi wake kulikoleta madhara makubwa.

Kiwango cha kupanda kwa gharama za maisha kwa kila mwaka cha zaidi ya asilimia milioni 11 na uhaba mkubwa sana wa chakula,mafuta na fedha za kigeni kumesababisha mamilioni ya Wazimbabwe kukimbilia katika nchi za jirani.