SiasaAfrika Kusini
Afrika Kusini yakabiliwa na shinikizo la kumkamata Putin
30 Mei 2023Matangazo
Chama cha Democratic Alliance (DA) kimepeleka shauri mahakamani kuhakikisha serikali inamkamata kiongozi huyo wa Urusi na kumkabidhi kwa ICC, ikiwa atakanya ardhi ya Afrika Kusini.
Serikali ya Afrika Kusini imekuwa ikikabiliwa na mkanganyiko wa kidiplomasia tangu Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) ilipotoa waranti wa kukamatwa kwa Putin, ambaye anatakiwa kuzuru taifa hilo kwa ajili ya mkutano wa BRICS mwezi Agosti.
Soma pia:ICC yataka Putin akamatwe
Afrika Kusini ambayo ni mwanachama wa mahakama ya ICC, ina uhusiano wa karibu wa kidiplomasia na serikali ya Moscow, na inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa wakuu wa nchi wa kundi la mataifa yanayoinukia kiuchumi BRICS, ambayo ni Brazil, Urusi, India, na China.