Matangazo
Uchaguzi huo wa Novemba Mosi unafanyika katika wakati ambao chama tawala cha ANC kinakabiliwa na shinikizo kubwa kufuatia vurugu zilizoikumba nchi hiyo zilizochochewa na hatua ya kukamatwa kwa rais wa zamani Jacob Zuma pamoja na uchumi unaoyumba kutokana na athari za janga la COVID-19. Rais Cyril Ramaphosa ameidhinisha kupelekwa wanajeshi 10,000 ili kuimarisha usalama kuelekea uchaguzi huo. Babu Abdalla amezungumza na mwandishi habari kutoka Afrika Kusini Bryson Bichwa na ambaye anaanza kwa kuelezea matayarisho ya kuelekea uchaguzi huo.