Afrika Kusini kupewa milioni €600 kufanikisha nishati safi
10 Novemba 2022Hatua hiyo ilitangazwa jana katika Mkutano wa kilele wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa wa COP27, unaoendelea katika mji wa Sharm Al-Sheikh nchini Misri. Afrika Kusini, mojawapo ya nchi 12 zinazoongoza kwa uchafuzi wa mazingira duniani, inazalisha takriban asilimia 80 ya umeme wake kupitia makaa ya mawe.
Mapema wiki hii katika mkutano huo, mataifa tajiri yaliidhinisha mpango wa uwekezaji wa dola bilioni 98 uliopigiwa upatu na mataifa yenye uchumi mkubwa zaidi barani Afrika ili kuachana na nishati inayochafua mazingira.
Kulingana na ripoti inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa iliyotolewa siku ya Jumanne, nchi zinazoendelea na nchi zinazoinukia kiuchumi zinahitaji uwekezaji wa zaidi ya dola trilioni 2 kila mwaka ifikapo mwaka 2030 ili dunia izuie mgogoro wa ongezeko la joto duniani.