1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Africa CDC yaitangaza mpox kuwa dharura ya afya ya umma

14 Agosti 2024

Kituo cha kudhibiti na kuzuwia magongwa barani Afrika, Africa CDC, kimeutangaza mlipuko wa ugonjwa wa homa ya nyani, au mpox kuwa dharura ya afya ya umma, na kusema hatua hiyo ni wito wa kuchukuwa hatua.

https://p.dw.com/p/4jQvv
Congo| Mpox
Africa CDC imetangaza dharura ya afya ya umma baada ya kuongezeka kwa visa wa ugonjwa wa mpox. Picha: AP/picture alliance

Kituo cha kudhibiti na kuzuwia magongwa barani Afrika,Africa CDC, kimeutangaza mlipuko wa ugonjwa wa homa ya nyani, au mpox kuwa dharura ya afya ya umma, na kusema hatua hiyo ni wito wa kuchukuwa hatua.

Mlipuko wa ugonjwa huo umeyakumba mataifa kadhaa ya Afrika, na hasa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, ambako ugonjwa huo ulioitwa monkeypox awali, uligundulika kwa mara ya kwanza mwaka 1970.

Soma pia: Hofu yatanda kufuatia mlipuko mpya wa homa ya nyani

Kulingana na data za CDC kufikia Agosti 4, kulikuwa na visa 38,465 vya mpox na vifo 1,456 barani Afrika tangu Januari 2022.

Tamko la CDC linakuja kuelekea mkutano wa dharura wa shirika la afya duniani, WHO, Agosti 14, kuamua iwapo litangaze dharura ya kimataifa kuhusiana na mlipuko huo.