1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfghanistan

Afghanistan yajadiliwa kimataifa

2 Mei 2023

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema, Jumuiya ya Kimataifa ina wasiwasi kuhusu uthabiti wa Afghanistan.

https://p.dw.com/p/4Qo2f
Afghanistan | Menschenrechtslage in Afghanistan
Picha: Ebrahim Noroozi/AP/dpa/picture alliance

Katibu mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aidha amesema kwamba hali ya nchi hiyo ndiyo ya mgogoro mkubwa kabisa wa kibinadamu inayoshuhudiwa duniani.

Tahadhari hiyo imetokana na mkutano wa Umoja wa Mataifa wa siku mbili uliomalizika mjini Doha ambapo imegusia masuala kadhaa ikiwemo kile kilichoitwa ugaidi,kushindwa kujumuishwa wanawake na wasichana pamoja na  kusambaa kwa visa vya usafirishaji madawa ya kulevya nchini Afghanistan.

Katika taarifa yake katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema pia atakutana na Taliban wakati mwafaka utakapowadia wa kufanya hivyo lakini wakati huo sio leo. Mkutano wa faragha wa  Doha umemalizika bila ya kutolewa tamko lolote rasmi la kuutambuwa utawala wa Taliban.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW