1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AfD yabainisha mikakati katika mkutano wake wa mwaka

Sylvia Mwehozi
29 Julai 2023

Kiongozi mwenza wa chama cha siasa kali, chama Mbadala kwa Ujerumani AfD, Alice Weidel, amesema chama hicho kinapaswa kuunda ushirikiano na vyama vinavyojitambua katika bunge la Ulaya ili kupambana na uhamiaji.

https://p.dw.com/p/4UXZC
AfD -mkutano mkuu
Mwanachama wa AfD Maximilian KrahPicha: dts Nachrichtenagentur/IMAGO

Kiongozi mwenza wa chama cha siasa kali, chama Mbadala kwa Ujerumani AfD,  Alice Weidel, amesema chama hicho kinapaswa kuunda ushirikiano na vyama vinavyojitambua katika bunge la Ulaya ili kupambana na uhamiaji.

Weidel ametoa matamshi hayo mbele ya wajumbe takribani 600 wanaohudhuria kongamano la kila mwaka la chama hicho lililoanza siku ya Ijumaa na kutarajiwa kumalizika siku ya Jumapili katika mji wa Magdeburg.

Ameeleza kuwa Umoja wa Ulaya umekosa demokrasia na mwelekeo na kwamba wataungana na vyama washirika ili kujenga ngome thabiti ya ulaya.

Wajumbe wa AfD wameunga mkono chama hicho kuungana na chama chenye itikada sawa cha Identity and Democracy ID katika bunge la Ulaya. Hii leo chama hicho kitaamua majina ya wagombea katika uchaguzi ujao kwenye bunge la Ulaya.