Adama Barrow aahidi kuweka ukomo wa muhula wa urais Gambia
8 Desemba 2021Barrow, ambaye ushindi wake wa mwaka wa 2016 ulihitimisha zaidi ya miaka 20 ya uongozi wa kidikteta, pia ameiahidi jamii ya kimataifa kuwa atafanya kazi kuhakikisha rais anachaguliwa kwa wingi mkubwa wa kura, badala ya kupitia mfumo wa sasa ambao mgombea anayeshinda kura nyingi katika kila jimbo la uchaguzi anachaguliwa kuwa rais.
Barrow hata hivyo hakuahidi kuwawajibisha wote waliohusika na uhalifu uliofanywa na serikali na mawakala wake chini ya uongozi wa kidikteta wa Yahya Jammeh.
Barrow, ambaye kuchukua kiti cha urais miaka mitano iliyopita kulimaliza zaidi ya miaka 20 ya udikteta, alipata zaidi ya asilimia 53 ya kura, kulingana na matokeo yaliyotolewa na tume ya uchaguzi. Mpinzani wake mkuu Ousainou Darboe alishika nafasi ya pili na asilimia 27.7.