Mauerfall
9 Novemba 2009Katika mwaka wa 20 tangu kuanguka kwa ukuta wa Berlin sherehe zinafanyika kote Ujerumani. Wakati huo huo lakini bado kuna manung'uniko ya hapa na pale kuhusu utaratibu wa muungano wa Ujerumani mbili pamoja na baadhi ya watu kuikumbuka iliyokuwa Ujerumani mashariki, DDR. Tarehe 9 Novemba 1989 hata hivyo, sio tu ni siku muhimu sana kwa historia ya Ujerumani, bali ni siku, ambayo wanastahili hasa kusherehekea kama siku ya kitaifa.
Ni siku yenye matukio ya kufurahisha na yanayogusa hisia, na pia ni siku inayoleta hali ya kuhuzunisha na pia yenye kutuliza mawazo. Hususan lakini tarehe 9 Novemba 1989 ni siku iliyosababisha siku njema kwa historia ya mpya ya Ujerumani na Ulaya kwa jumla. Haikuangusha tu mfumo mbaya usiokuwa wa haki , lakini ilisababisha kupatikana kwa muungano wa Ujerumani mbili ambazo kwa muda wa miaka 40 zilitengana. Tarehe 9 Novemba pia ni siku ambayo kwa muda wa muongo mmoja kumekuwa na manung'uniko kuhusu muungano huo , pamoja na haki na uhuru wa kila mtu, ambapo katika jamii iliyowazi mtu anaweza kujihisi na kufurahia hali ya ushindi.
Pamoja na hayo lakini katika muda huu wa miaka 20 baadhi bado wameendelea kukumbuka jambo moja au jingine. Sio upande wa Ujerumani ya magharibi , na haikuwa mwanasiasa yeyote ambaye amefanikisha siku hii. Walikuwa ni wananchi wenyewe wa DDR, ambao katika mitaa iliyochakaa katika taifa lao lililozingirwa na ukuta, hakuna kilichokuwa kinapata changamoto kubwa zaidi , kuliko haki yao wanayostahili.
Ndio sababu maandamano ya wiki kadha ya amani yaliweza kuuangusha ukuta uliojengwa kwa saruji na nondo za chuma , na hii ni historia ya kikatiba katika demokrasia na wanastahili kuuangusha. Na hapa kila mmoja leo anastahili kufikiri juu ya hali ya muungano wa Ujerumani, kuhusiana na kile kinachodaiwa kuwa ni kuanguka kwa uchumi wa upande wa mashariki ama haki yao ya kuwa uhuru na kuingia katika mchakato wa kidemokrasia, kuweza kuchagua chama wakitakacho, kile ambacho kinaweza kurejesha hali ya iliyokuwa kisoshalist ambayo waliipenda.
Ni dhahiri kwamba si kila kitu ambacho kimekwenda sawa katika muda wa miaka hii 20 ya muungano. Ahadi za haraka haraka hazikuweza kutekelezwa. Ujenzi mpya wa haraka haraka , pamoja na uchumi wa soko huru katika nchi hii iliyoharibika kiuchumi ya iliyokuwa Ujerumani mashariki ya zamani DDR, imeleta tu kwa watu wengi hali mbaya ya maisha. Pamoja na hayo lakini katika hatua hii ya maendeleo hakuna njia mbadala. Pamoja na hayo kutokana na mapinduzi haya katika DDR sio tu kumekuwa na mabadiliko ya msingi katika nchi lakini pia utaratibu mzima duniani kote.
Tarehe 9 Novemba ni siku ambapo historia ya uchokozi, ambayo ilikuwa inachochea mizozo ya kimataifa kati ya kambi ya magharibi na mashariki ilimalizika, na pia kuleta hali ya utulivu. Na kwamba hii leo ulimwengu umekuwa katika utata zaidi, haueleweki na unaohitaji ufafanuzi zaidi, kuna mkono pia wa kuanguka kwa ukuta huu.
Mwandishi Koch: Marc / ZR / Kitojo Sekione.
Mhariri: Mohammed Abdul Rahman.