Vifo vilivyotokana na matetemeko Afghanistan vyafikia 2,053
8 Oktoba 2023Matangazo
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kabul, msemaji wa Mamlaka ya Taifa ya Kukabiliana na Maafa (ANDMA) amesema kutokana na matetemeko hayo ya Jumamosi, vijiji takribani 13 vimeteketea kabisa. Amesema zaidi ya watu 1,200 wamejeruhiwa. Idadi ya waliokufa ni ya awali kwa kuwa kazi ya uokozi bado inaendelea waokoaji. Jumamosi asubuhi katika kipindi kifupi matetemeko manane ya ardhi yalitikisa eneo la mpakani karibu na Iran.Kulingana na Shirika la Afya Duniania WHO, takriban watu 4,200 wameathiriwa na nyumba zipatazo 600 zimeharibiwa.