SiasaUswisi
2023: Uchumi unatarajiwa kuimarika
20 Januari 2023Matangazo
Lagarde ameyasema haya huko Davos Uswisi kunakoendelea kongamano la uchumi duniani wakati ambapo kuna matumaini ya nchi kukwepa mdororo wa uchumi. Mkuu huyo amesema nia ya Benki Kuu ya Ulaya ni kuurudisha uchumi hadi asilimia mbili na kuchukua hatua zote zinazostahili ili kufikia lengo, licha ya changamoto ya mfumuko wa bei unaoshuhudiwa hivi sasa. Kulingana na makadirio yake, Benki Kuu ya Ulaya inatarajia kuwepo na ukuaji wa uchumi katika kanda hiyo kwa asilimia 0.5. Matumaini hayo ingawa yenye tahadhari yameanza wakati ambapo bei za juu za nishati zilizopanda mwaka jana kutokana na vita nchini Ukraine, zikianza kushuka.