Matangazo
Makundi ya watu yamiminika katika barabara za mji mkuu wa Sudan Khartoum baada ya baraza la kijeshi linaloongoza nchini humo na muungano mkuu pinzani kutia saini makubaliano ya mwisho ya serikali ya mpito.Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Horst Seehofer apendekeza wanaotafuta hifadhi kutoka Syria wanapaswa kurejeshwa nchini mwao ikigundulika kuwa wamekuwa wakirejea nchini humo na waziri mkuu Boris Johnson kutumia ziara yake ya Ufaransa na Ujerumani kuwaambia viongozi wa Umoja wa Ulaya kwamba bunge la Uingereza haliwezi kuzuia Uingereza kujitoa kutoka umoja huo.